Ikiwa yamebaki masaa machache kuelekea kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na Lake Fm redio ya Jijini Mwanza, akaunti ya Instagram ya redio hiyo imevamiwa na watu wanaosadikika kuwa ni wahuni wa mtandaoni.
"Siku hizi mitandao ya kijamii ina nguvu sana hususani kwenye kusambaza habari, hivyo nadhani wameamua kuingilia akaunti yetu baada ya kuona namna ambavyo tunaitangaza show ya Usiku wa Mshike Mshike inayofanyika leo". Uongozi wa Lake Fm umefafanua na kuongeza;
"Tunapenda kuwaambia Wananzengo wetu kwamba show hiyo itafanyika kama kawaida na tayari Khadija Omar Kopa amewasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kuwapa burudani hivyo wasishtuke kutoona posts zetu kwenye mtandao wa Instagram kwani tunapatikana Facebook na Twitter @lakefmmwanza".
Mbali na akaunti ya redio kuibiwa, pia akaunti za Instagram za wafanyakazi wa redio hiyo pamoja na wasikilizaji wake waliokuwa wakipost kuhusu show ya Mshike Mshike zimeibiwa ambapo wataalamu wa redio hiyo wanashughulikia tatizo hilo.
Show ya Mshike Mshike inafanyika leo alhamisi Oktoba 27,2016 katika kiwanja cha nyumbani Villa Park Rerort kuanzia saa moja jioni kwa kiingilio cha shilingi 7,000 kabla ya saa tano usiku na shilingi elfu kumi baada ya saa tano usiku ambapo bendi ya Ogopa Kopa Classic pamoja na wasanii mbalimbali akiwemo Fatina Khamis kutoka bendi ya Big Star watakuwepo. Na BMG
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni