.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 15 Oktoba 2016

BOURNEMOUTH YAICHAMBUA KAMA KARANGA TIMU YA HULL CITY

Bournemouth imeipa kipigo kikali Hull City cha magoli 6-1 na kuifanya kupata ushindi wa tatu mfululizo wakiwa nyumbani, huku Hull ikiendeleza kutokushinda katika michezo sita.

Charlie Daniels alikuwa wa kwanza kufungulia mvua hiyo ya magoli, baada ya mpira wa adhabu wa Ryan Mason kurudi, na kisha baadaye Steve Cook kusawazisha goli hilo.

Cook alifunga kwa kichwa na kuifanya Bournemouth kuongza tena katika mchezo huo, kabla ya Stanislas kufunga la tatu na kisha kufunga la nne.

Callum Wilson alifunga goli la tano katika dakika za mwisho kabla ya Dan Gosling kukamilisha karamu hiyo ya magoli kwa kufunga la sita.
                Charlie Daniels akishangilia goli lake la kwanza kwa kukirukia teke kibendera
     Steve Cook akiwa juu baada ya kupiga kichwa mpira uliojaa wavuni na kusawazisha goli
                 Mpira uliopigwa na Charlie Daniels ukitinga wavuni na kuandika goli la pili 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni