Wataalamu wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wanatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kukagua Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Huu ni utaratibu wa CAF ambako baada ya muda hutembelea nchi wanachama kuangalia maendeleo ya miundombinu ya mpira wa miguu kabla ya kupandisha hadhi ya viwanja kwa ajili ya michuano ya kimataifa inayosimamiwa na kuendeshwa na CECAFA, CAF na FIFA.
Ukaguzi huo unafanyika wakati Tanzania inasubiri majibu ya Uwanja wa Sokoine wa Mbeya ambao ulikwiisha kukaguliwa na mapendekezo ya uboreshwaji kutolewa ili uweze kupandishwa hadhi ya matumizi ya kuchezwa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani, michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA.
Viwanja ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini Tanzania hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar; Kaitaba wa Kagera, Azam Complex na Uwanja Mkuu wa Taifa vya Dar es Salaam.
Endapo CCM Kirumba utapitishwa, kutakuwa na nafasi ya kuruhusu kuchezwa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA.
Kirumba inaingia kwenye orodha ya viwanja vya Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya, Kaitaba wa Kagera ambavyo vilikwisha kukaguliwa na sasa vinasubiri kupitishwa ili kutumika kimataifa. Ujio wa viwanja hivyo, utapanua wigo wa Tanzania kuandaa michuano mikubwa katika ngazi ya timu za taifa kimataifa.
Timu 12 zinatarajiwa kushiriki Ligi ya Taifa ya Wanawake inayotarajiwa kuanza Novemba mosi, mwaka huu kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Soka la Wanawake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoridhia tarehe hiyo.
Tayari klabu zimeagizwa kuzingatia jina kuenenda na namba za jezi mgongoni ili kuepusha mkanganyiko wa wachezaji wakati wa ligi hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
kwa tarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/626-ligi-ya-wanawake-tanzania-bara
LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Oktoba 8, 2016 kwa michezo mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Wakati African Lyon itaikaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam JKT Ruvu yenyewe itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.
kwa tarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/625-vpl-viwanja-vitatu-kuwaka-moto-kesho
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni