Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akishiriki katika zoezi la kuvuruga bustani ambazo zimelimwa karibu na vichoteo vya maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
Na Mathias Canal, Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi ameshiriki katika
zoezi la kuvuruga bustani ambazo zimelimwa karibu na vichoteo vya maji
kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
Dc Ndejembi ameamua kufanya
zoezi hilo la kuharibu bustani hizo baada ya wananchi Karibu na vyanzo
hivyo vya maji baada ya wananchi wanaoishi karibu na maeneo hayo kuamua
kulima bustani za mboga mboga kwa kutumia maji ya bomba ambayo hupaswa
kusukumwa kujaza tanki la kutunzia maji.
Uharibifu huo
umefanywa na Dc Ndejembi huku akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na
usalama ya Wilaya ya Kongwa ikiwa ni sehemu ya utendaji Kazi na
kuhamasisha ufanisi wa ukuzaji wa kilimo chenye tija.
Dc
Ndejembi ameamua kufanya hivyo baada ya kubaini kuwa wananchi hao
wamekuwa wakifungulia maji ya bomba na hatimaye kumwagika chini ili
kumwagilia bustani zao nyakati za usiku muda ambao pampu inasukuma maji
kuelekea kwenye Tanki lililopo makao makuu ya Wilaya ambalo hujazwa ili
maji hayo yaweze kuwahudumia wakazi wa Mjini Kongwa.
Kadhia
hiyo ya kufunguliwa maji kwa kificho nyakati za usiku imesababisha
kutojaa kwa Tanki hilo Hali ambayo imesababisha kukosekana kwa maji
katika maeneo ya Wilaya ya Kongwa.
Kabla ya kuanza kwa zoezi
hilo la kuvuruga bustani hizo Dc Ndejembi aliamuru wananchi
waliohudhuria katika zoezi hilo kuchuma mboga mboga zilizokuwepo katika
bustani hizo sambamba na kuchota maji yote ambayo yalikuwa yamehifadhiwa
katika bustani hizo kwa ajili ya kumwagilia bustani hizo.
Vichoteo vilivyotobolewa katika bomba kuu ambalo linalekea Mjini vipo
katika kijiji cha Ibwaga ambavyo vilianzishwa maalumu kwa ajili ya
kusaidia wanakijiji wa vijiji vya karibu
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni