Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka nje ya Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa ziara ya kibinafsi Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali walihudhuria katika swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja leo,ambapo Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,na ujumbe wake waliswali kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakiwa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja leo,ambapo Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,na ujumbe wake waliswali kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 28/10/2016.







Hakuna maoni :
Chapisha Maoni