Nchi ya Haiti imeanza zoezi la
kuhamisha wakazi waliopo kwenye maeneo hatarishi kutokana na kimbunga
kikubwa kiambatanacho na mvua kiitwacho Matthew, kinachotisha kuleta
maafa, mafuriko kikiwa na upepe wenye kasi ya kilomita 240 kwa saa.
Kimbunga hicho ni kukikubwa
kulikumba eneo la Atlantic kwa karibu muungo mmoja, kinatarajia
kuikumba Haiti na Jamaica hapo kesho, Kituo cha Taifa Cha Vimbunga
cha Marekani kimeeleza.
Wakazi wa maeneo hatarishi wameanza
kuweka akiba ya mahitaji yao muhimu, huku Waziri Mkuu wa Jamaica
akiwataka wananchi kujiandaa kukabiliana na janga hilo kabla ya muda
wa kufanya hivyo hauajaisha.
Watu wakifanya manunuzi ya mahitaji yao muhimu ya kutosha ili kujiwekea akiba kabla ya kimbunga Matthew hakijanza
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni