Timu ya taifa ya Italia imepambana
kiume ikitokea nyuma na kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya
Macedonia, katika mchezo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe
la dunia.
Katika mchezo huo, Andrea Belotti,
aliipatia Italia goli la kuongoza akimalizia mpira wa kona, lakini,
Ilija Nestorovski, akaisawazishia Macedonia baadaye.
Wenyeji Macedonia iliwashtua Italia
pale ilipopata goli la pili kupitia kwa Ferhan Hasani hata hivyo Ciro
Immobile alisawazisha na kisha kuongeza la tatu katika dakika za
mwisho.
Ciro Immobile akifunga goli kati ya magoli mawili aliyoyafunga katika mchezo huo
Ferhan Hasani akifunga goli la pili la Macedonia lililowapagawisha mashabiki wa taifa hilo
Ferhan Hasani akifunga goli la pili la Macedonia lililowapagawisha mashabiki wa taifa hilo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni