Picha zote na Fredy Njeje/Story na Mwana Libeneke wa Funguka Live Dickson Mulashani
Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF) imezindua kampeni kwa jina BINTI WA KITAA eneo la Pakacha kata ya Tandale wilaya ya Kinondoni itakayodumu kwa mwaka mmoja yenye lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba pamoja na ndoa za utotoni nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa (CVF) Ndg. George David amesema kama mtanzania ameguswa na tatizo hili ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hata katika kipindi hiki cha utandawazi hivyo anaamini kupitia kampeni hii, elimu itawafikia walengwa kwa namna ya tofauti na licha ya kupunguza tatizo hili itasaidia kulimaliza kabisa.
“Inauma sana kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi 5 duniani zinazotambulika kwa janga la mimba pamoja na ndoa za utotoni, hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo” alisema George.
BINTI WA KITAA imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 17 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani na inatarajiwa kuzuru mikoa zaidi ya 10 nchini huku ikiwa na agenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kuweza kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa Kitanzania.

Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazowapelekea mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,hii ndio iliyosababisha kampeni hii kuzinduliwa mtaa wa Pakacha Tandale kwani.Kadhalika mmoja kati ya mabinti waliohudhuria katika uzinduzi huo Zawadi Isihaka ameomba wazazi kufuatilia maendeleo na kuwa karibu na watoto wao ili kuweza kuyagundua mapema mabadiliko ya tabia pamoja na kuwapa elimu ya makuzi sambamba na kutokuwa wakali kupitiliza kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo waratibu wa eneo ambao ni Tandale Youths, Applemacbooks Company,wakazi wa eneo la Pakacha ,Tandale, waandishi wa habari pamoja.
Sambamba na uzinduzi huo katika kata ya Tandale,Ndg. George David ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono kampeni hii ili kuweza kuwasaidia mabinti kwani ni wazi kuwa hili limekuwa sehemu kubwa ya kuzalisha wimbi kubwa la watoto wa mitaani, vifo wakati wa kujifungua, athari za kisaikolojia na kiuwanyima mabinti nafasi ya kupata haki yao ya msingi ya elimu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni