.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 23 Oktoba 2016

KASI YA UKUAJI WA UCHUMI NCHINI YAVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Norio Shoji Nyumbani kwake Bara bara ya Haile Selassie Jijijini Dar es salaam.
Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kutoka Japan ukiongozwa na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Norio Shoji wa Pili kutoka Kulia ukibadilishana mawazo na Balozi Seif.
Bwana Norio Shoji akimueleza Balozi Seif shauku ya Kampuni yake kutaka kuwekeza vitega Uchumi Nchini Tanzania kulingana na mazingira na rasilmali zilizopo
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Norio aliyepo kati kati mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika nyumbani kwake Bara bara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam. Wa kwanza kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Koichi Kawaji. (Picha na – OMPR – ZNZ.)

Kasi kubwa ya uchumi wa Tanzania inayoonekana kupanda kwa haraka katika kipindi kifupi imeanza kutoa ushawishi mkubwa kwa Makampuni na Taasisi za Kimataifa kuonyesha dalili za kutaka kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi na maendeleo ili kuunga mkono kasi hiyo.

Rais wa Kamuni ya Kimataifa ya Uwekezaji Vitega Uchumi ya Koyo kutoka
Tokyo Nchini Japan Bwana Koichi Kawaji akiuongoza Ujumbe wa Viongozi
Sita wa Kampuni hiyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Bara
ara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam.

Bwana Koichi Kawaji alisema tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na Wataalamu wa masuala ya Uchumi Duniani umebaini kwamba kasi ya uchumi wa Taifa la Tanzania unaongoza ikilinganishwa na Mataifa yaliyomo ndani ya Bara la Afrika kwa hivi sasa .

Kiongozi huyo wa Kampuni ya Kimataifa ya Koto alifahamisha kwamba
Tanzania ni nchi ya kwanza Barani Afrika yenye muelekeo mpana wa Uchumi wake kukuwa kwa haraka ukifananishwa na Nchi ya Singapore Bwana Koichi alisema wataalamu wa Kampuni ya Koyo wamelazimika kufanya ziara ya makusudi katika azma ya kujionea kasi hiyo Nchini Tanzania na kuangalia maeneo ambayo Taasisi hiyo ya Uwekezaji inaweza kutumia fursa zilizopo katika kusaidia ukuaji wa Uchumi wa Tanzania.

Alieleza kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilmali za kutosha za
Kiuchumi ambazo kwa namna nyingi Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchini
wanaweza kutumiwa vyema katika njia ya kuingia ubia na Serikali, Makampuni au hata Watu binafsi wenye sifa na shauku ya kuwekeza.

Rais huyo wa Kamuni ya Kimataifa ya Uwekezaji Vitega Uchumi ya Koyo kutoka Tokyo Nchini Japan Bwana Koichi alielezea furaha yake kutokana na utulivu mkubwa na Amani iliyotanda Nchini Tanzania katika kipindi kirefu sasa.

Alisema amani na utulivu huo kwa kiasi kikubwa ndio iliyozaa mafanikio
makubwa ya Uchumi yanayoendelea kupatikana na hatimae kuchangia
mapato ya Taifa sambamba na kupunguza umasikini lakini kwa njia nyengine pia umezuia mfumko wa bei unaotoa afueni ya maisha bora kwa
Wananchi walio wengi.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishauri Serikali ya Japani kupitia ujumbe wa Kampuni hiyo ya Koyo kuangalia maeneo ambayo Taasisi na Makamuni ya Nchi hiyo yanaweka
kuwekeza. 


Balozi Seif alisema Tanzania imepakana na Bahari kuu eneo ambalo Japan
kutokana na kuendelea Kiviwanda inaweza kusaidia Taa luma katika Mpango wa kulielekeza Taifa la Tanzania kuwa Nchi ya Viwanda ifikapo Mwaka 2025.

Alisema Tanzania bado ina fursa nzuri ya kujifunza Taaluma ya Uvuvi wa Bahari kuu kwa kuanzishwa Viwanda vya usindikaji bidhaa zinazotoka na
mazao ya Baharini kama Samaki wa aina mbali mbali pamoja na zao la Mwani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni
hiyo ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibat itakuwa tayari kutoa msaada wowote utakaohitajiwa na Kampuni
hiyo wakati itakapofikia hatua ya kutaka kuwekeza miradi yake Visiwani Zanzibar.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
23/10/2016.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni