.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 11 Oktoba 2016

MAGAVANA WA BENKI YA DUNIA WAHIMIZA USHIRIKISHWAJI

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Katibu Mkuu Bw. Dotto James (kulia) wakiandika pointi muhimu wakati Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim, alipowahutubia Mawaziri wa Fedha na Makatibu wakuu (Magavana) kutoka nchi za Kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini Washington DC-Marekani.
Wajumbe wa Tanzania waliohudhuria mkutano wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakimsikiliza kwa makini Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (hayupo pichani) wakati Mawaziri wa Fedha na makatibu wakuu (Magavana) kutoka nchi wanachama wa Taasisi hizo kutoka Bara la Afrika, walipokutana kama kamati, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dotto James, wakifuatilia kwa makini mkutano wa Magavana wa Benki ya Dunia kutoka Barani Afrika uliohudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiwa na Waziri wa Fedha wa Swaziland Bw. Martin Dlamini wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu (Magavana) kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika, mkutano uliomshirikisha pia Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani, Christine Lagarde (hayupo pichani), Jijini Washington DC, Marekani.
Wataalamu wa Fedha na Uchumi Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakisikiliza kwa makini mkutano wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, ukisimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bi. Christine Lagarde (Hayupo Pichani) ambaye aliwambukusha
wajumbe wanaoziwakilisha nchi zao kuwa umasikini bado ni changamoto kubwa na unasababisha vikwanzo vingi katika kukuza maendeleo na ustawi wa nchi wanachama, Jijini Washington DC-Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakibadilishana mawazo kabla ya kukutana na uongozi wa Juu wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya Afrika, Jijini Washington DC nchini Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya Afrika, Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe Hayupo pichani), Jijini Washington DC-Marekani. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu akifuatiwa na Naibu Gavana wa Benki hiyo Dkt. Natu Mwamba.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (aliyenyoosha mkono)
akielezea jambo wakati Ujumbe wa Tanzania Ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kulia kwake, walipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Africa Group I Bw. Abebe Aemro Selassie (Hayupo pichani) ambapo Gavana alieleza kuhusu uchumi wa sasa wa Tanzania pamoja na Hali ya uchumi unavyokua kwa kiasi cha kuridhisha, Jijini Washington Marekani.
Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato,
akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kitabu Chenye maelezo mbalimbali ya miradi inayotekelezwa nchini Tanzania kwa ufadhili wa shirika hilo, ambapo Japani imeahidi kuendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kuendeleza miundombinu ya barabara na sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akiwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James (kushoto) wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato, wakati Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango ulipokutana na Mkurugenzi huyo ambaye ameahidi kuwa Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii, Jijini Washington DC, Marekani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni