Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali ndani nje ya nchi wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela akizungumza mapema leo,alipokuwa akimkaribisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Katika kongamano hilo kauli mbiu yake ni “Uwekezaji katika tafiti zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia.
Dkt Mwele alieleza pia Mada zitakazojadiliwa ndani ya kongamano hilo kuwa zitajikita zaid kwenye maeneo kama vile 1. Mkakati wa kuboresha afya ya uzazi, ya mama, watoto wachanga na vijana. 2. Magonjwa sugu yasiyoambukiza na changamoto zake,3. Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria,4. Usalama wa Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi,5. Mkakati wa afya moja katika kudhibiti magonjwa ya milipuko,pamoja na 6. Magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya 200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya 200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo,kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo kufungua Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kati ni Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni