Konagamano hilo limelenga kuwahamasisha wanawake kujikomboa kiuchumi ambapo wanawake mbalimbali waliofanikiwa kiujasiriamali, kibiashara na kielimu watakuwepo kuzungumza na wanawake Jijini Mwanza ambapo kiingilio itakuwa elfu 40 tu na utapata elimu, burudani pamoja na chakula.
"Atakuwepo Shekha Nasser ambaye ni mmiliki wa Shear Illusion na Mwanzilishi wa Manjano Foundation ambaye amefanikiwa kwenye biashara, atakuwepo Mkandarasi Maida Waziri ambaye amekuwa mkandarasi na amefanikiwa pamoja na Biubwa Ibrahim ambaye ana Kampuni inaitwa Namaingo Agri_Busness Agency ambayo inawawezesha watu mbalimbali katika masuala ya kilimo na wengine wengi". Amefafanua Masimba.
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba akiwa ndani ya 102.5 Lake Fm Mwanza akizungumzia Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu ndani ya Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni