- Kwa mara ya kwanza Merck kutoa takriban tembe milioni 10 kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Ivory Coast.
Merck (MerckGroup.com),
kampuni kubwa ya sayansi na teknolojia, imetangaza leo kuwa imetoa
msaada wa tembe milioni 500 za kutibu ugonjwa wa minyoo ya kichocho
unaodhuru kwa siri kwa Shirika la Afya Duniani (WHO). Katika shule
inayopatikana takriban kilomita 25 magharibi kaskazini mwa Abidjan,
wawakilishi kutoka Merck, WHO na Wizara ya Afya ya Ivory Coast
wametangaza kwa sauti moja uzinduzi wa usambazaji wa dawa hiyo nchini
Ivory Coast.
Juhudi
za Merck za kupambana na ugonjwa wa kichocho zilianza mwaka 2007 na
zinahusisha nchi 35 barani Afrika. Zaidi ya wagonjwa milioni 100,
hususan watoto wa shule, wametibiwa hadi leo hii. “Tumejizatiti
kuendelea kutoa tembe milioni 250 kila mwaka hadi ugonjwa huu mbaya
uishe,” alisema Belén Garijo, mwanabodi wa Bodi ya Utendaji ya Merck na
Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma ya Afya. “Kutoa msaada wa tembe milioni
500 za praziquantel leo hii kunaonyesha hatua kubwa tuliyoipiga katika
kufanikisha lengo hili.” Garijo aliongezea.
Katika
sherehe iliyofanyika katika shule ya msingi ya kijiji cha Attinguie,
wawakilishi wa Wizara ya Afya Ivory Coast na British Schistosomiasis
Control Initiative (SCI) walisimamia tembe za praziquantel za matibabu
ya ugonjwa wa kichocho kwa watoto. Watoto hupokea kati ya tembe moja
hadi tano, kulingana na urefu wao. Pia, walimu waliwaelezea sababu za
ugonjwa wa minyoo ya kitropiki. Kwa lengo hili, Merck imetoa msaada wa
jumla ya vijitabu 20,000 vya kuelimisha kwa WHO kwa ajili ya Ivory
Coast.
Kwa
mujibu wa WHO, zaidi ya asilimia 20 ya idadi ya watu nchini Ivory Coast
wanahitaji matibabu. Hadi leo, shirika la maendeleo la Marekani USAID
pamoja na Schistosomiasis Control Initiative (SCI) wameiunga mkono
serikali ya Ivory Coast katika vita dhidi ya ugonjwa wa kichocho.
Kama
mwanachama wa Global Schistosomiasis Alliance, Merck imekuwa
ikishirikiana na mashirika yote mawili tangu 2014. Ndani ya ushirikiano
huu, kampuni hii imetoa msaada wa tembe milioni 3.6 kwa WHO kwa mwaka
2016. Kwa sababu hiyo, Ivory Coast imenufaika kwa mara ya kwanza
kutokana na ushirika kati ya Merck na WHO. Mwaka wa 2017, Merck itatoa
tembe milioni 6.5 kwa WHO kwa ajili ya nchi ya Afrika Magharibi.
Ugonjwa
wa kichocho unaathiri takriban watu milioni 260 duniani kote. Kiwango
cha maambukizi kipo juu zaidi kwa watoto, na madhara yake ni makubwa
zaidi. Ugonjwa huu wa vimelea unaathiri ukuaji, husababisha ulemavu wa
kujifunza, na husababisha upungufu wa damu mwilini. Merck inatoa msaada
wa tembe za praziquantel kwa WHO kama sehemu ya uwajibikaji wake katika
jumuiya na ndani ya Afya, mojawapo ya shughuli zake za mkakati wa
uwajibikaji wa shirika.
Praziquantel ni matibabu bora yanayovumiliwa na
yenye ufanisi zaidi kufikia sasa kwa ugonjwa wa kichocho. Aidha, Merck
inatoa usaidizi wa mipango ya kielimu na programu za kuhamasisha,
kufanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa kichocho kwa kila watoto wachanga
na kushirikiana na washirika katika Umoja wa Kupambana na Kichocho
Duniani (Global Schistosomiasis Alliance).
Distributed by APO on behalf of Merck.
Vyombo vya habari Mawasiliano:
Friederike Segeberg +49 6151 72-4081
Friederike.Segeberg@
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni