Mongela amewataka vijana kubuni njia mbalimbali halali za kuwaingizia kipato ikiwemo ujasiriamali badala ya kukaa bila kazi huku wakijivunia kuwa kwenye vyama vya siasa.
Amesema ni vyema wanaoingia kwenye siasa wakahakikisha wana shuguli za kufanya ambapo amewasihi wajasiriamali wakiwemo Machinga kuwa tayari kufanya biashara zao katika maeneo yaliyoainishwa na kwamba watakaotii hilo, watanufaika moja kwa moja na mikopo inayotolewa na halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Naye Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Odila Batimayo, kwa niaba ya umoja huo, amempongeza Rais John Magufuli kutokana na utendaji mwema wa kazi ikiwemo kuanza kutimiza ahadi zake ndani ya miezi tisa ya uongozi wake kama vile ununuzi wa ndege, mabehewa, ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na mpango wa elimu bure nchini.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana, Hussein Kimu, amebainisha kwamba lengo la mkutano huo ni kuyapongeza makundi mbalimbali yakiwemo machinga, mamantilie na bodaboda kutokana na mchango wao katika kufanikisha ushindi katika uchaguzi wa mwaka jana, ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe wa mkutano huo wamepata fursa ya kuchangia damu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela (katikati), akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa Baraza Kuu Maalumu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, uliofanyika "Gandhi Hall" Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela, akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana, Hussein Kimu, akizungumza kwenye mkutano huo
Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Odila Batimayo, akisoma taarifa ya UVCCM Nyamagana kwenye mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Wajumbe pamoja na Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Taswira ya mkutano wa Baraza Kuu Maalumu ya UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, ikiwa ni sehemu ya kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kuanzishwa kwa umoja huo, "UVCCM DAY" kitaifa. Imeandaliwa na BMG
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni