.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 13 Oktoba 2016

MKUU WA WILAYA IRINGA, MH. KASESELA AZINDUA KINGA TIBA YA KICHOCHO

Pichani Mkuu wa wilaya Iringa, Mh Richard Kasesela akiendesha zoezi la kugawa dawa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Umsalaam iliyopo manispaa ya Iringa.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela leo amezindua kampeni ya kuwanywesha watoto dawa ya Kinga tiba kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani Iringa. 

Shule zote za msingi katika wilaya ya Iringa zitapata dawa na kuwanywesha watoto wote ilikujikinga na ugonjwa wa kichocho.
Pichani Mkuu wa wilaya Iringa, Mh Richard Kasesela akiendesha zoezi la kugawa dawa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Umsalaam iliyopo manispaa ya Iringa. 

Mh Kasesela alisema " wazazi wawaruhusu watoto wao kupata kinga tiba kwani wataondokana na ugonjwa hatarishi. wataalamu wametuambia hazina madhara yoyote ili mradi mtoto awe amekula". Shule zote zitakazotoa dawa zitahakikisha watoto wana pata chakula kabla hawajapewa.
Zoezi hili litafanyika wiki mbili na kuhakikisha kila mtoto anapata Kinga tiba. Pia alipata fursa ya kuwafafanunulia baadhi ya wazazi waliokuwa na shaka na dawa hizo .

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni