Ripoti ya Shirika la Save the
Children, imesema kuwa mtoto wa kike mmoja mwenye umri chini ya miaka
15 huolewa kila baada ya sekunde saba duniani.
Utafiti wa Save the Children
umeonyesha watoto wa kike wenye umri hadi wa miaka 10, hulazimishwa
kuolewa na wanaume wenye umri mkubwa mno kwenye mataifa ya
Afghanistan, Yemen, India na Somalia.
Mapigano, umasikini na migogoro ya
kibinadamu imeelezwa kuwa ni sababu kuu zinazochangia mtoto wa kike
kuingia kwenye ndoa za utotoni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni