Mtu anayedaiwa kuwa ni gaidi wa
kundi la al-Shabaab amepigwa risasi na kufa baada ya kumchoma kisu
askari wa kikosi cha GSU nje ya ubalozi wa Marekani uliopo eneo la
Gigiri Jijini Nairobi nchini Kenya.
Ubalozi wa Marekani umethibitisha
kutokea kwa tukio hilo jana, ambapo hakuna mtumishi wa ubalozi huo
aliyejeruhiwa, na kuviagiza vyombo vya habari kupata taarifa zaidi
kwa serikali ya Kenya.
Mtuhumiwa huyo wa ugaidi inadaiwa
kuwa alikuwa akilazimisha kungia kwenye Ubalozi wa Marekani nandipo
alipozuiwa na maafisa polisi wa Kenya kwenye geti na kisha alichomoa
kisu na kumchoma askari polisi kabla ya kupigwa risasi na kufa.
Maafisa wa upelelezi wa Marekani wa kikosi cha FBI wakiuchunguza mwili wa mtu aliyeuwawa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni