Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza mara baada ya kupokea
msaada wa tofali 2300 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa
katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru
akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakati wa
kukabidhi madawati kwa ajili ya shule ya msingi Msamadi.
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiongozana na Mkurugenzi wa Mamlaka
ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA),Joyce Msiru
wakitizama ujenzi wa madarasa matatu unaoendelea katika shule ya msingi
Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Mkuu
wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa
shule ya Msamadi ,Seseama Bayo mara baada ya kupokea matofali 2300
yaliyotolewa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi
(MUWSA).
Mafundi wakishusha tofali zilizotolewa na MUWSA kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa .wengine ni watumishi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi.
Jengo jipya lenye madarasa mawili katika shule ya msingi Msamadi ambalo kwa kiasi kukamilika kwake kutasaidia kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa shuleni hapo.
Moja ya madarasa yaliyopo shuleni hapo kama linavyoonekana ambapo wanafunzi wamekuwa wakikaa chumba kimoja kwa idadi kubwa kuliko uwezo wa darasa.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni