.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 10 Oktoba 2016

MWASAPILI: ‘TULIENI’ POINTI TATU NI ZETU

MLIZI wa kutumainiwa kwenye kikosi cha Mbeya City fc, Hassan Mwasapili amewataka mashabiki wa timu yake kutulia na kutokuwa na hofu yoyote na mchezo ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba Sc uliopangwa kuchezwa jumatano hii kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo, Mwasapili aliweka wazi kuwa hana presha yoyote na mchezo wa jumatano kwa sababu anaifahamu vizuri Simba hasa ukizingatia kuwa huu utakuwa ni mchezo wake wa tano kucheza dhidi ya timu hiyo tangu kupanda daraja kwa kikosi cha Mbeya City.

“Huu utakuwa mchezo wangu wa tano kucheza dhidi ya Simba Sc,naifahamu vizuri najua nguvu yao iko kwenye eneo gani la uwanja, siwezi kusema mengi juu ya matokeo yao msimu huu ni hakika wameanza vizuri lakini kuna jambo moja muhimu kuwa mechi zote waalizoshinda wamecheza nyumbani, jumatano hii huu ni wakati wao mgumu zaidi kwa sababau sasa wanacheza ugenini na hii ndiyo nafasi yetu sisi kupambana nao na kuwafunga” alisema.

Akiendelea zaidi Mwasapili alitanabaisha kuwa,matokeo ya pointi nne kwenye michezo miwili ya City iliyopita yametosha kuhifadhi nguvu za kutosha kukabiliana na kikosi cha Simba Sc hivyo hakuna shaka yeyote kuwa nafasi ya ushindi ipo kwa timu yake amabayo itakuwa ikicheza kwa nguvu zote kutokana na uwepo wa sapoti ya mashabiki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni