.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 3 Oktoba 2016

NCHIMBI ‘AIMALIZA’ MWADUI FC

BAO LA dakika ya 27 kipindi cha kwanza lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa kati Ditram Nchimbi, lilitosha kuhitimisha dakika 90 za mchezo namba 50 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliozikutanisha Mbeya City fc dhidi ya wageni Mwadui Fc kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya matokeo yaliyomuacha kocha wa Mwadui Fc akitangaza kujiuzuru kufundisha pia kujihusisha na mchezo wa soka hapa nchini.

Kwenye mchezo huo uliokuwa na kasi ya aina yake, timu zote zilianza dakika 45 za kwanza kwa nguvu kubwa iliyoacha mashambilizi ya kila mara pande zote mbili lakini uimara wa walinda milango, Owen Chaima na Shaban Kado ulifanya washambuliaji wa timu zote kushindwa kufunga mabao ya mapema.

Dakika ya 27, mpira ulioanzia upande wa kulia kwa John Kabanda aliyefanikiwa kuupitisha vizuri katikati ya uwanja kwa nahodha Kenny Ally, ulifanikiwa kufika kwenye miguu ya Ditram Nchimbi ambaye akiwa nje kidogo ya eneo la 18 la Mwadui Fc alifumua shuti kali lililomshinda kipa Kado na kutinga wavuni moja kwa moja,kuandika bao la kwanza kwa City lililodumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili, kocha wa City Kinnah Phiri alifanya mabadiliko kwa kumtoa, Joseph Mahundi na nafasi yake kuchukuliwa na Hamidu Mohamed pia alimtoa Omary Ramadhani na kuingia Salvatory Nkulula huku Rajab Zahir aliyepata majeraha akimpisha Ramadhani Chombo, mabadilliko yaliisaidia timu yake kuimarisha safu ya kiungo na hatimaye kufanikiwa kukamilisha dakika 90 matokeo yakibaki kama yalivyokuwa.

Mara baada ya mchezo kocha msaidizi Mohamed Kijuso, alisema wachezaji wake wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo jambo lililochangia kupatikana kwa ushindi huu.

“Mchezo ulikuwa mzuri, vijana wamecheza kwa kufuata maelekezo ya Mwalimu, hili limetusaidia kuibuka na ushindi,hatukuwa vizuri kipindi cha pili lakini safu yetu ya ulinzi ilisimama imara kufuta makosa yote, huu ni wakatri mwingine wa kuijiandaa na mchezo ujao kwa sababu tayari tuna nguvu na ari kubwa kufuatia ushindi wa leo “alisema.

Katika hatua nyingine kocha wa Mwadui Fc , Jamhuri Kihwelo alitangaza kujiuzuru kuifundisha timu hiyo huku akiapa kutokujihusisha tena naa mchezo wa soka nchini kwa kile alichookita kuchoshwa na upindishaji wa sheria 17 za soka aliyodai unafanywa kwa makusudi na waaamuzi wa soka licha ya kukiri kutokuwa na tatizo lolote na bao alifungwa kwenye mchezo wa jana.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni