Mchezaji mkongwe wa zamani wa timu
ya taifa ya Cameroon, Rigobert Song Bahanag, amepatwa na tatizo la
kiharusi na kulazwa katika kituo cha Yaoundé Emergency.
Song ambaye pia aliwahi kuwa kapteni
wa timu ya taifa ya Cameroon, alianza kuugua siku ya jumapili, kwa
mujibu wa chanzo cha karibu na familia yake.
Raia wa Cameroon wametumia mitandao
ya kijamii kumuombea Song apone haraka, ambapo tangu alazwe bado yupo
katika hali ya mahututu.
Beki huyo mwenye nguvu aliwahi
kuzichezea timu za Ligi Kuu ya Uingereza za Liverpool na West Ham,
vile vile alizichezea Metz na Lens za Ufaransain France na
Galatasaray ya Uturuki.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni