Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wa Tabata Kimanga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kuondolewa kwa takataka zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali na mkandarasi aliyepewa tenda ya kuziondoa.
Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Dar es Salaam juzi mkazi wa eneo hilo, Mfaume Wakwetu alisema katika maeneo mengi ya Tabata Kimanga kunatakataka nyingi zimerundikwa kando ya barabara bila kuondolewa na wahusika.
"Takataka nyingi zimerundikwa katika eneo la stendi ya mabasi hapa Tabata Kimanga na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa stendi hiyo na wapita njia" alisema Mfaume.
Aliongeza kuwa takataka zilitolewa majumbani huwekwa katika madampo madogo yaliyoanzishwa kandio ya barabara lakini mkandarasi aliyepewa tenda hiyo hushindwa kufika kwa wakati kuziondoa hivyo kuwa kero kwao.
Aliongeza kuwa kutokana na takataka hizo kuachwa kwa muda mrefu bila kuondolewa husambaa hadi kwenye mifereji ya maji taka ambayouziba na kusababisha maji kushindwa kupita na kutoa hahrufu kali na kusababisha mafuriko mvua zinaponyesha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni