Tottenham imemaliza rekodi ya kuanza
vyema Ligi Kuu ya Uingereza kocha Pep Guardiola, kwa kuibuka na
ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester City katika dimba la White
Hart Lane.
Guardiola alikuwa ameshinda michezo
yake sita ya awali, lakini katika mchezo wa leo City ilijikuta
ikizidiwa kila idara na Tottenham ambao sasa wamebakia kuwa timu
pekee ambayo haijafungwa katika Ligi Kuu ya Uingereza.
Spurs walitawala mchezo huo tangu
mwanzo ambapo walipata goli lao la kwanza katika dakika ya tisa baada
ya Aleksandar Kolarov kujifunga katika harakati za kuokoa krosi
iliyopigwa na Danny Rose, huku Dele Alli akifunga goli pili.
Beki wa Manchester City Aleksandar Kolarov akiwa anajutia goli la kujifunga
Dele Alli akiangalia shuti lake alilopiga likimshinda kipa na kuiandikia Tottenham goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni