Bingwa wa Uzito wa Juu duniani Tyson
Furry amesema bado anaendelea na ngumi, baada ya awali kuashiria kuwa
amejiuzulu mchezo huo.
Bondia huyo Muingereza ambaye
alijiondoa katika pambano la Oktoba 29 la dhidi ya Wladimir Klitschko
kutokana na masuala ya kiafya, alituma twitti isemayo “Mimi ni bora
na nimejiuzulu."
Hata hivyo saa tatu baadaye Fury,
28, alirejea katika mitandao ya jamii na kusema alikuwa anatania,
bado hajajiuzulu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni