.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 10 Oktoba 2016

UZINDUZI WA BODI YA WADHAMINI WA MFUKO WA MAJI

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (Mb.) akisoma hotuba ya Uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Maji wakati akizindua Bodi hiyo leo katika ofisi za Wizara ya Maji na Umwagiliaji Makao Makuu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (Mb.) kulia kwake akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Emmanuel Kalobelo, wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Maji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Maji, Vincent Mrisho akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Maji, Sekretariati ya Mfuko na Menejimenti ya Wizara ya Maji.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (Mb.) leo amezindua Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Maji. Mfuko huu umeanzishwa kisheria kupitia Kifungu 44 (1) cha Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na. 12 ya 2009. Mfuko huu ulianzishwa ili kuwa na chanzo endelevu cha fedha za uwekezaji katika miradi ya maji Uzinduzi huo umefanyika katika ofisi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji Makao Makuu zilizopo Ubungo Maji. 

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bodi hiyo, Waziri Lwenge amesema Wajumbe wa Bodi wanatakiwa kuwa wabunifu, waadilifu na wachapakazi ili kuleta mabadiliko ambayo yataiwezesha nchi yetu Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa kati ya viwanda. 

Aidha, Waziri Lwenge alitoa msisitizo kwa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Maji kuwa, hataweza kuivumilia bodi isiyoweza kuhimili kasi ya kufikia dhamira ya serikali iliyotajwa katika Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020. Bodi inatarajiwa kusiamia kikailifu matumizi ya fedha na kubuni vyanzo vya mapato ya kukuza Mfuko ili uweze kuongeza tija katika uwekezaji na miradi ya maji kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi Pili Bodi ifanye kazi kwa ufanisi, welei na uzalendo; kwa misingi ya haki bila ubaguzi wala upendeleo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Vincent Mrisho, alisema kwamba Bodi itajitahidi kufanya kazi kwa karibu na kushirikiana na Sekretariati ili kuweza kuleta ufanisi na kujitahidi kuwasilisha taarifa sahihi za bodi.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni