Jamii ya Wamasai kutoka Wilaya ya Simanjiro wakiwa katika sherehe za kuhama rika ambapo wananchi 600 walihama rika na kuamia rika la wazee maarufu kama Korianga |
Viongozi wa Mila wa jamii ya Wamasai wametakiwa kusuluhisha na kutatua migogoro ya ardhi,maeneo ya malisho pamoja na wizi wa mifugo ili kuepusha uvunjifu wa amani na kuzorota kwa maendeleo kunakosababishwa na migogoro hiyo.
Hayo yameelezwa na Wazee wa Mila Peter Toima na Lemamiye Shininii wakati wa sherehe za kuhama rika ambao Maelfu wa vijana kutoka Wilaya ya Simanjiro wanahamia rika la wazee na kukabidhiwa wajibu wa kuwa wasuluhishi katika jamii.
Wazee hao Walisema kuwa jukumu la kutatua migogoro linapaswa kufanywa na Wazee hao wapya na kuepuka kuitwisha serikali mzigo mkubwa wa migogoro ambayo wangeweza kuitatua .
Kwa upande wao Vijana waliohama rika na kuingia rika la wazee Oreka Mlolo na walisema kuwa kazi kubwa iliyoko mbele yao ni kuhakikisha kuwa jamii inaishi kwa amani ,kudumisha umoja na ushirikiano ambazo ni tunu muhimu kwa jamii ya Wamasai.
Mmoja wa Kinamama ambao Waume zao wameama rika Loema Thadey alisema kuwa mila hiyo hutumika kupima uaminifu wa Wanandoa iwapo Mwanamke anachepuka basi anaweza kupoteza maisha.
Jamii ya Wamasai ni jamii yenye tamaduni yenye nguvu iliyodumu kwa muda mrefu na kuenziwa licha ya changamoto ya utandawazi uliomeza tamaduni nyingi za Kiafrika na kuleta utamaduni wa nchi za Magharibi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni