Jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon itakuwa mwenyeji wa Mbeya City ya Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda Fc kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo utaofanyika Uwanja wa Manungu, ulioko Turiani – Mvomero.
Majimaji itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Majimaji huko Songea. Michezo yote mitano hapo juu itaanza saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki lakini mchezo kati ya Azam FC na JKT Ruvu itaanza saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam huko Chamazi-Mbagala Dar es Salaam.
Jumapili itakuwa ni zamu ya kinara wa ligi hiyo, Simba ambayo itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Tanzania Prisons itapambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Michezo yote ya Dar es Salaam, mfumo wa kuingia utabaki kuwa ni uleule wa kutumia kadi za Selcom kununua tiketi za kielekroniki. Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Uhuru ni Sh 30,000 kwa Jukwaa Kuu (VIP-A), VIP-B na C Sh 20,000 na mzunguko ni Sh 5,000 wakati Kiingilio Uwanja wa Azam ni Sh 10,000 kwa VIP na Mzunguko ni Sh 3,000.
Wakati mzunguko wa tano wa Ligi Daraja la Kwanza ukitarajiwa kuendelea kesho Jumamosi na keshokutwa Jumapili, Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeagiza makamishna na wakuu wa vituo kuzuia wachezaji wote ambao hawana leseni kutocheza.
Hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14 (16), inayosema: “Wachezaji wote watatambulika kwa kutumia leseni zao zitakazotolewa na kuidhinishwa na TFF. Mchezaji yoyote ambaye hatakuwa na leseni hataruhusiwa kucheza katika mchezo husika.”
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/641-ligi-daraja-la-kwanza-kuendelea-kesho
LIGI YA TAIFA YA WANAWAKE
Ligi ya Taifa na Wanawake itaanza Novemba 1, 2016 kama ilivyopangwa awali kwa kushirikisha timu 12 zilizopangwa kwenye makundi mawili yenye majina ya ‘A’ na ‘B’. Kila kundi lina timu sita.Timu za kundi A lina timu za Viva Queens ya Mtwara, Fair Play ya Tanga, Mlandizi Queens ya Pwani pamoja na Mburahati Queens, Evergreen Queens na JKT Queens za Dar es Salaam wakati kundi B zimo Marsh Academy ya Mwanza, Baobab Queens ya Dodoma, Majengo Women ya Singida, Sisters FC ya Kigoma, Kagera Queens ya Kagera na Panama FC ya Iringa.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
http://tff.or.tz/news/640-ligi-ya-taifa-ya-wanawake

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni