Watu wapatao 52 wamekufa na wengine
wengi wamejeruhiwa katika mkoa wa Oromia nchini Ethiopia baada ya
kufanyika maandamano wakati wa tamasha la kidini.
Serikali ya Ethiopia imesema baadhi
ya watu wamekufa baada ya kukanyagana baada ya polisi kufyatua mabomu
ya machozi, kurusha risasi za mipira na kutumia virungu.
Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn
amesema waandamanaji walipanga kufanya ghasia walizofanya na
kusababisha watu kuanguka kwenye bonde na kufa.
Waandamanaji wakiangaliana uso kwa uso na askari wakati wa maandamano hayo
Askari wakitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha waandamanaji
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni