Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe.Said Djinnit. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Oktoba, 2016.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Omary Mjenga (wa kwanza kushoto), Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Ally Ubwa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Bw. Djinnit (hawapo pichani).
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Bw.Djinnit mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni