Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.
Katika majaribio hayo walijitokeza jumla ya vijana 406 kutoka sehemu tofauti na jiji hilo kabla ya kuchujwa na kufikia 29 na hatimaye kupatikana 10, ambao wataingia kwenye mchujo wa mwisho utakaofanyika Azam Complex mwezi ujao.
Mchujo huo wa mwisho utashirikisha vijana wengine 50, waliochaguliwa kwenye maeneo mengine saba nchini ambayo Azam FC tayari imeshayatembelea, ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro iliyojumuisha pia vijana wa mkoa wa jirani wa Dodoma pamoja na Visiwani Zanzibar (Unguja na Pemba).
Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, anayeendesha zoezi hilo amefurahishwa na wingi wa vijana walijitokeza jijini Mbeya huku akiridhishwa na vipaji vyao akidai kuwa huo ni mwanga mzuri wa kutengeneza kikosi bora kwa manufaa ya Azam FC na Taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa ripoti ya mpango huo, mpaka sasa Azam FC imeshawafanyia usaili vijana 2,999 kwenye maeneo yote nane waliyotembelea, wakichaguliwa 60 pekee kwa ajili ya kuingia katika mchujo wa mwisho wa fainali utaotoa vijana bora watakaounda timu hiyo.
Kwa taarifa nyingine za kina kuhusu program hii, tunakuomba uendelee kufuatilia vyanzo vyetu mbalimbali vya habari (www.azamfc.co.tz , mitandao yetu wa Facebook na Twitter ‘Azam FC’).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni