Timu ya Bayern Munich itamaliza
katika nafasi ya pili katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kundi D baada ya
kupata kipigo cha kushtukiza cha magoli 3-2 kutoka kwa FC Rostov ya
Urusi.
Timu hiyo ya Ligi Kuu ya Urusi
ilipata ushindi wake huo wa kwanza kati Ligi ya Mabingwa Ulaya katika
mchezo huo uliochezwa kwenye hali ya hewa ya nyuzi joto -4.
Kwa matokeo hayo FC Rostov inakuwa
timu ya kwanza ya Urusi kuwahi kuifunga timu kubwa ya ligi ya
Bundesliga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Cristian Noboa akishangilia goli lake la mpira wa adhabu lililofanya matokeo kuwa 3-2
Katika mchezo mwingine Atletico
Madrid imeibuka na ushindi wa magoli mawili kwa bila dhidi ya PSV
Eindhoven, magoli yaliyofungwa na Gameiro na Griezmann.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni