Harry Kane amerejea tena dimbani
baada ya kuwa majeruhi na kuisawazishia Tottenham goli na kuifanya
timu hiyo kuwa timu pekee ambayo haijafungwa katika Ligi Kuu ya
Uingereza, baada ya kutoka sare ya 1-1 na Arsenal.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa
ya Uingereza alikuwa benchi tangu aumie Septemba 18, aliifungia
Tottenham kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha pili baada ya Kevin
Wimmer kujifunga katika kipindi cha kwanza.
Harry Kane akipiga mpira wa penati uliozaa goli la kusawazisha la Tottenham
Homa ya mchezo huo ilipanda na kuamsha ghadhabu kama inavyoonekana hapa



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni