.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 15 Novemba 2016

KIMETA CHAUA NYUMBU 90 MONDULI

Na Woinde Shizza,Arusha

Zaidi ya nyumbu 90 na swala 15 wamekufa katika eneo la mapito ya
wanyamapori, lililopo kwenye kata ya Selela wilayani Monduli mkoani
Arusha.nadaiwa kuwa wanyama hao wameangamia kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta ulioibuka katika ushoroba huo wa Selela, unaoziunganisha mbuga za Tarangire na Hifadhi ya Ziwa Manyara, pia umeangamiza idadi kubwa ya wanyama wa kufugwa hasa ng'ombe, mbuzi na kondoo wapatao 60, huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta amesema baada ya matukio ya  wanyamapori kuanguka ghafla na kufa kwa wingi na baadaye mifugo pia  kuanza kuangamia, uongozi wa wilaya ulipeleka sampuli za mizoga hiyo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi na ambaye alithibitisha  uwepo wa kimeta.

“Tunahofia kuwa kimeta sasa kitakuwa kimesambaa maana wanyama kama  nyumbu wana tabia ya kuhamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine, hivyo  si ajabu wamepeleka ugonjwa huu maeneo mengine," alisema.

Ofisa Mifugo wilayani Monduli, Salum Omar amethibitisha kufa kwa  ng'ombe, mbuzi na kondoo kadhaa katika eneo lake na kuongeza kuwa hivi  sasa wameanza taratibu za kutoa chanjo dhidi ya maambukizi ya kimeta kwa mifugo iliyobaki.

“Lakini kuna haja pia ya kuhakikisha kuwa wafugaji, wengi wakiwa ni wa  jamii za Kimasai, wanapewa elimu juu ya mlipuko wa ugonjwa huu, maana wengi  wanakula mizoga ya mifugo yao iliyokufa,” alionya ofisa mifugo huyo.

Kwa kawaida binadamu akigusa mzoga wa mnyama aliyekufa kwa kimeta,
huweza kupata maambukizo hayo. Sasa wafugaji wa Monduli wanakwenda mbali zaidi, kula nyama iliyoathirika.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Selela, Julius Loiboseki ameomba msaada kwa  serikali iwasaidie kuzuia mifugo kutoka maeneo ya jirani ili isiingizwe  kwenye maeneo yao hadi pale tatizo litakapotatuliwa.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Diwani wa Kata hiyo ya Selela, Cuthbert  Meela ambaye alifafanua kuwa wilaya ya Monduli haijawahi  mlipuko wa kimeta au ugonjwa wowote ule mkubwa wa kutishia maisha ya
watu na wanyama.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni