Bondia David Haye amemrushia konde
mpinzani wake, Tony Bellew katika mkutano wa waandishi wa habari huku
akimponda kuwa hana uwezo wa kupambana naye.
Mabondia hao ambao pambano lao
lisilo la kutetea mkanda wowote litafanyika Machi 4 katika ukumbi wa
02 Arena Jijini London nusura wazichape kavukavu.
Licha ya kumrushia konde Bellew,
Haye alimponda mpinzani wake huyo na kusema hahitaji maandalizi
yoyote zaidi ya kwenda kujirusha klabu na wakikutana atamdunda.
Bondia David Haye akimrushia konde bondia Tony Bellow
Mabondia David Haye na Tony Bellow wakiamuliwa
HUNITISHI BWANA: Tony Bellow akimsemea mbovu David Haye baada ya kumponda




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni