Jose Mourinho na wachezaji wake wa
Manchester United waliamua kuweka kando hali yao ngumu katika ligi,
na kuhudhuria mlo wa jioni ulioandaliwa na shirika la UNICEF na
kusaidia kuchangishwa paundi 215,000 za msaada.
Mourinho pekee alisaidia kukusanywa
paundi 30,000 kwa kuuza vitu vyake, saini yake, sweta la Adidas, nguo
ya juu ya mazoezi pamoja na kitambaa cha skafu, na kisha kuamua
kuitoa saa yake aliyovaa inayouzwa paundi 16,000.
Kocha Jose Mourinho akivua saa yake aliyoitoa ipigwe mnada kuchangisha fedha
Wachezaji wa Manchester United wakiwa katika picha ya pamoja
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni