Timu ya Manchester United imemaliza
ukame wa kutokushinda michezo minne ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa
kuifunga Swansea City kwa magoli 3-1.
Manchester United iliutawala mchezo
huo tangu mwanzoni na kufanikiwa kufunga magoli 3-0 hadi mapumziko,
Paul Pogba akifunga goli la shuti kali huku Zlatan Ibrahimovic
akitupia mawili.
Mike van der Hoorn aliifungia goli
Swansea kipindi cha pili huku wageni Manchester United wakionekana
kutotishiwa na safu ya Swansea, katika mchezo huo ambao kocha Jose
Mourinho aliushuhudia akiwa jukwaani baada ya kufungiwa.
Zlatan Ibrahimovic akiachia shuti lililoza goli lake la kwanza hapo jana
Zlatan Ibrahimovic akishangilia goli lake kwa kuruka teke la kung fu
Kipa Fabianski akiruka bila ya mafanikio kuzuia mpira wa shuti kali la Paul Pogba




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni