.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 16 Novemba 2016

MEYA SEONGNAM KUSAPOTI TFF

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana Novemba 15, 2016 alimtembelea Mstahiki Meya wa Jiji la Seongnam, Jae-myung Lee kumshukuru kwa namna ambavyo ameipokea timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys.

Serengeti Boys walioko Korea kwa michezo ya kirafiki ya kimataifa ambako Jiji la Seongnam ni mshirika wa klabu ya Seongnam FC ambao ndio wenyeji wa timu yetu ya vijana ambayo ilifanya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa.

Katika mazungumzo kocha huyo, Meya Jae-myung Lee aliiakikishia TFF kuwa jiji lake litaendelea kushirikiana na shirikisho katika kuendeleza mpira wa vijana wakike na wakiume.

Katika kumtembelea Meya huyo, Rais Malinzi aliambatana na Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na benchi nzima la ufundi, linaloongozwa na Kocha Bakari Nyundo Shime na msaidizi wake, Muharami Mohammed Sultan pamoja na Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya soka la vijana, Kim Poulsen.

Baadaye jioni ya Novemba 15, 2016 Rais Malinzi alikutana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Korea Kusini (KFA), Chung Mong-Gyu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Hyundai.

Rais wa KFA Mong-Gyu naye alihakikishia TFF kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Korea litasaidia kuendeleza soka la vijana Tanzania sambamba na kusaidia mafunzo ya makocha..


TFF YAMSIMAKISHA MCHEZAJI KAGERA SUGAR
 

Kutokana na malalamiko ya timu ya mpira wa miguu ya Panone Fc juu ya ushiriki wa mchezaji Christopher Mahanga katika Ligi ya TFF ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 iliyoko Kundi A, Kituo cha Bukoba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesimamisha ushiriki mchezaji Christopher Mshanga katika mashindano yanayoendelea mpaka uchunguzi wa suala lake utakapokamilika.
 

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji italifanyia kazi suala hilo na taarifa itatolewa.


Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
 

http://www.tff.or.tz/news/679-tff-yamsimakisha-mchezaji-kagera-sugar

BURIANI MSAFIRI RAMADHANI MSAFIRI
 

Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Msafiri Ramadhani Msafiri.
 

Taarifa za kifo hicho kilichotokea usiku wa kuamkia Novemba 15, mwaka huu akiwa njiani kwenda Hospitali ya Milagwe, Kampala nchini Uganda, imetolewa na Katibu Mkuu wa KRFA, Saloum Chama ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji TFF.


Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
 

http://www.tff.or.tz/news/678-buriani-msafiri-ramadhani-msafiri

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni