Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga wakifuatila mchezo wa fainali katika kata ya Ikwea ambapo mshindi alipata ng'ombe mmoja na mshindi wa pili akipokea zawdi ya mbuzi mmoja ambapo zawadi zote hizo zimetolewa na mbunge huyo.
Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga akikabidhi ng'ombe kwa mshindi wa kwanza katika kata ya Ikwea ambapo mshindi wa kwanza ilikuwa timu ya Ugenza FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.
Na fredy mgunda,mafinga
MASHINDANO ya Mpira wa miguu yaliyodhaminiwa na Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa yanayojulikana kama Mgimwa Cup yamefika tamati katika tarafa ya Sadan yenye kata tatu ambazo Ikwea,Sadan na Igombavanu na fainali zote zilifanyika katika kata husika ambapo kila mshindi wa kata alipata ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alipata mbuzi moja,hivyo jumla ya ng’ombe tatu na mbuzi tatu zimetolewa katika tarafa ya Sada.
Katika fainali ya kwanza ilichezwa katika viwanja vya kijiji cha Ugenza iliyopo katika kata ya Ikwea ilishuhudiwa timu ya Ugenza FC wakiibamiza timu ya Ikwea FC kwa goli 1-0 katika mchezo wa vuta nikuvute.
Baada ya mchezo huo katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Hassani Mtenga alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki wa michuano hiyo ambapo mshindi wa tatu ambaye ilikuwa timu ya Victoria FC alizawadiwa mipira miwili, mshindi wa pili Ikwea FC walipata mbuzi mmoja na mpira mmoja na mshindi wa kwanza ambaye ni Ugenza FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.
Mtenga aliwaasa wachezaji kuithamini michezo kwa kuwa sasa ni ajira hivyo wanajukumu la kujituma na kuipa kipaumbe michezo na kuacha tabia za kukaa kwenye vijiwe na vilabu ambako wanapoteza muda kwa kujadili mambo yasiyo ya msingi.
Akifunga mashindano hayo mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba vijana hao wajiunge katika vikundi ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo ambapo itawasaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa.
"Mimi kama Mbunge ambaye nimetokea katika kata hii nimevutiwa sana na ninaguswa na matatizo yanayowakabili vijana hasa katika ajira na michezo hii imefungua ukurasa mpya kwenu nawaomba vijana wote mjiunge katika vikundi ili tuweze kuwasaidia kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali,"alisema makilagi.
Mgimwa alisema kuwa ligi hiyo itakuwa ikichezwa kila mwaka huku shughuli za maendeleo kwa vijana hao zikiendelea kama alivyowaahidi kuwa atawatafutia fedha kwa ajili ya maombi yao waliyotoa kwa mbunge huyo.
Naye mgeni rasmi katika fainali ya kata ya Sadan Yohanies Kaguo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) alishuhudia timu ya Kibada fc ikiibuka mshindi kwa kuifunga timu ya Ihanzutwa fc goli moja kwa bila na kuwakabidhi washindi ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alikabidhiwa mbuzi mmoja.
Kaguo aliwataka wachezaji wa timu zote za kata ya Sadan kutunza vipaji vyao kwa kuwa ndio ajira yao na kuongeza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DR John Pombe Magufuli wamedhamili kuvithamini vipaji vyote nchini na kuvigeuza kuwa ajira kwao.
“Angalia wakina Thomas Ulimwengu,Mbwana Samatta na wachezaji wengi wanavyonufaika na vipaji vyao vya michezo hivyo na nyinyi mnatakiwa kujituma ili kufikia mafanikio waliofika baadhi ya hao wachezaji” alisema kaguo.
Kwa upande wa kata ya Igombavanu mgeni rasmi alikuwa katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi (CCM) Jimson Mhagama naye alishudia timu ya Lugoda fc ikiibuka mshindi na aliikabidhi timu hiyo zawadi ya ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alipewa mbuzi mmoja.
Mhagama alimpongeza mbunge wa jimbo la Mufindi Mahamood mgimwa kwa jitihada za kuinua na kuibua vipaji vipya kutoka kwenye jimbo lake.
"Kutoa ng’ombe mmoja na mbuzi mmoja kila kata sio jambo dogo linahitaji kujipanga sana hivyo mnapoona mashindano kama haya mnapaswa kuyakimbilia na kushiriki kikamili ili kuibuka washindi na kuweka historia kwa kuwa mabingwa" alisema mhagama
Mashindano ya Mgimwa cup yatafanyika katika tarafa zote za jimbo la Mufindi kaskazi na jumla ya ng’ombe kumi na moja na mbuzi kumi na moja zitatolewa kwenye jimbo la Mufindi kaskazini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni