Serikali ipo kwenye mpango wa kuanza utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya afya katika kila kata nchi mzima ili kumaliza changamoto ya upungufu huo uliopo kwa sasa katika maeneo mengi.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo hapo Jana wakati wa ziara yake wilayani Pangani.
Alisema kuwa mpango huo unatarajiwa kuanza utekelezaji wake kuanzia mwaka ujao wa fedha kwa kila Halimashauri kujengewa kituo kimoja cha afya katika ngazi yakata .
Alisema kuwa kupitia mpango huo serikali itaweza kwa kiasi fulani kufikia lengo la lake iliyojiwekea la kila kata kuwa na kituo cha afya ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa licha ya utekelezaji wa Sera ya afya kutiliwa mkazo katika maeneo mengi hapa nchini bado mpaka sasa Tanzania mzima inavituo vya afya 440 pekee.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya yaPangani Zainab Abdallah alisema kuwa wilaya hiyo inakata 14 lakini ina kituo cha afya kimoja hali inayosababisha changamoto ya utoaji wa huduma.
“Wilaya yetu maeneo kata nyingine zimetenganishwa na mto Pangani hivyo kutoka na hali hiyo tumelazimika kujenga kituo cha afya katika kata za ngambo ili tuweze kuwahudumia wananchi wote” alisema Dc huyo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni