Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Ruaha kwenye semina iliyoelezea malengo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani ambapo kati ya hao, vijana 50 wamepata semina ya mwongozo wa kuwa mabalozi wa malengo hayo (Global Goals Champions).
Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
























Hakuna maoni :
Chapisha Maoni