Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi Anna Muro amesema kuwa msaada huo utasaidia kuwawezesha wanawake Waweze kushiriki kwenye maendeleo ya jamii .
Akizungumza katika kituo hicho kinacholelea watoto 30 wenye watoto ambao walipata mimba katika umri mdogo na kushindwa kuendelea na masomo ambapo wanasaidiwa na kituo hicho kupata elimu ya ufundi wa ushonaji na mapishi ili kupata stadi zitakaowasaidia kujikwamua kimaisha.
Anna amesema kuwa watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya usafirishaji wa binadamu jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu na haki za watoto hivyo amewataka Jamii na serikali kupiga vita usafirishwaji wa watoto.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama amewataka watoto wanaoishi katika kituo hicho kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata kujiendeleza kielimu na kukua kiuchumi ili kutokomeza umasikini na mimba za utotoni kwa watoto wa kike.
Muasisi wa kituo hicho Martina Simon Siara ameshukuru ugeni kutoka UN na EU uliofika kituoni hapo kwa ajili ya kutazama shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho pamoja na kuwaunga mkono ili waweze kuongeza tija katika kuisaidia jamii.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni