Naibu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lidwino Mgumba pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi hilo wametembelea kiwanda kinachotarajiwa kutengeneza magari ya Zimamoto na Matrekta (EQUATOR SUMA JKT Co. Ltd) kilichopo Ruvu eneo la Mlandizi mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo ambayo aliifanya mapema leo asubuhi, Naibu Kamishna Jenerali alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Ndg. Robert Mangazeni na kufanya mazungumzo ya kuona ni jinsi gani wanaweza kutatua tatizo la kukabiliana na majanga ya moto hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo alimuakikishia Naibu Kamisha Jenerali “kiwanda hiki kitakapo zinduliwa tutaweza kumaliza changamoto za uchache wa vitendea kazi inayolikabili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji“ Alisema Mkurugenzi huyo.
Naye Naibu Kamishna Jenerali alishukuru pamoja na kumuahidi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo “tutashirikiana kwa karibu na kwa kitaalamu kwani sisi ndiyo wenye dhamana ya kuokoa maisha na mali za umma wa watanzania katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengine“ Alisema Naibu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni