Maelfu ya waandamanaji wameingia
mitaani katika miji kadhaa ya Marekani kupinga ushindi wa urais wa
Donald Trump.
Watu hao wengi wao wamekuwa wakipaza
sauti wakisema “Trump sio rais wangu” na wengine wakichoma moto
masanamu ya mfanyabiashara huyo aliyeshinda urais.
Trump atakuwa rais wa 45 wa Marekani
baada ya kupata ushindi wa kushtukiza dhidi ya mgombea wa Democratic,
Bi. Hillary Clinton.
Waandamanaji wakiwa na mabango huku sanamu ya Donald Trump ikiwa imening'inizwa juu
Waandamanaji wakichoma moto bendera ya Marekani
Maandamano hayo pia yaliambatana na vitendo vya kuchomwa magari




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni