Polisi nchini Israeli imewakamata
watu 12 kwa tuhuma za kuwasha moto wa nyika uliounguza maeneo kadhaa
ya mji wa Haifa kwa siku nne.
Vikosi vya zimamato vimefanikiwa
kuudhibiti moto huo kaskazini mwa mji wa Haifa, ambao wakazi wake
wapatao 80,000 waliagizwa kuuhama.
Hata hivyo maafisa wa zimamoto
wamesema kuwa bado kuna moto midogo midogo inayoendelewa kuzimwa
katika maeneo tofauti.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni