Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe kutoka Serikali ya Finland (hawapo pichani), Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Judica Omary.
Waziri
wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen
(kulia), akizungumza katika Mkutano kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo
katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Biashara, Mawasiliano na
Nishati, kati ya Tanzania na Finland . Kushoto ni Balozi wa Finland
nchini Tanzania Pekka Hukka, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa
Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe
kutoka Serikali ya Finland (kushoto) na wenyeji wao kutoka Tanzania
(kulia) wakiwa katika mkutano wa pamoja wakijadili kuhusu masuala ya
Ushirikiano wa Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na
Nishati, kati ya pande hizo mbili, Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati), akipeana
mkono na Balozi wa Finland nchini Tanzania Pekka Hukka (kulia), baada
ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Tanzania na Finland kuhusu Ushirikiano
wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati, Biashara, Kilimo na Mawasiliano.
Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Finland Kai
Mykkanen, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango, jijini Dar es Salaam
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni