Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushoto akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Kiuchumi ya MCC Overseas LTD ya China unaoongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Leo Zou aliyeko upande wa kulia kwenye Hoteli ya Sheraton Mjini Beijing.
Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum.
Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Kiuchumi ya MCC Overseas LTD ya China Bwana Leo Zou kushoto akiagana na Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Mjini Beijing.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechapuzwa kuendelea kuongeza nguvu zaidi katika uimarishaji wa Miundombinu ili iende sambamba na kasi iliyopo ya kuongezeka kwa miradi ya Utalii pamoja na ile ya Sekta nyengine inayowekezwa katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechapuzwa kuendelea kuongeza nguvu zaidi katika uimarishaji wa Miundombinu ili iende sambamba na kasi iliyopo ya kuongezeka kwa miradi ya Utalii pamoja na ile ya Sekta nyengine inayowekezwa katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Zanzibar.
Chapuzo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Kiuchumi ya MCC Overseas LTD ya China Bwana Leo Zou wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye Hoteli ya Sheraton Mjini Beijing.
Bwana Leo Zou ambae Kampuni yake ndio iliyotiliana Saini Mkataba na Kampuni ya Penny Royal kwa ajili ya Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Hoteli ya Kimataifa ya Daraja la Tano {Five Star } Amber Resort Zanzibar katika Kijiji cha Matemwe alisema Zanzibar hivi sasa inaeleweka vyema katika ramani ya Dunia.
Mwenyekiti huyo wa Kampuni ya MCC Overseas alimueleza Balozi Seif na Ujumbe wake uliopo Nchini China kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku Tano kwamba Zanzibar lazima iwe makini katika kuandaa mipango imara ya miundombinu itakayokidhi mahitaji halisi ya ongezeko kubwa la wageni.
Bwana Leo Zou alisema siku chache alizokuwepo Visiwani Zanzibar ameshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya wageni wanaoingia kwa ajili ya shughuli za Utalii pamoja na Uwekezaji tokea kufunguliwa njia za Uwekezaji katika miradi mingi ya sekta ya Utalii.
Mwenyekiti huyo wa Kampuni ya MCC - Overseas alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Uongozi wa Taasisi hiyo umeridhika na mazingira mazuri yaliyopo Zanzibar yanayotoa fursa za uwekezaji kwa Taasisi na Makapuni ya Kigeni kushawishika kutaka kuwekeza miradi hyao.
Alisema MCC Overseas mbali ya kujenga mradi wa Hoteli wa Amber Resort Zanzibar lakini pia iko tayari kuwekeza miradi yake mengine katika sekta ya Umeme na huduma za Maji safi na salama.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Miradi ya Mafuta na Gesi Asilia pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar ni miongoni mwa juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uimarishajhi wa miundombinu.
Balozi Seif hatua hiyo itahamasisha wawekezaji katika sekta ya usafiri wa Anga kuongeza safari zao za moja kwa moja hadi Zanzibar kutoka nchi ya Falme za Kiarabu { UAE } na zile wa Bara la Asia ili kuongeza kasi ya Utalii.
Aliueleza Ujumbe wa Viongozi hao wa MCC Overseas kwamba watalii na wageni wanaoingia kwa wingi Zanzibar wakati huu ni wale wanaotoka katika Mataifa ya Ulaya hasa Nchi ya Italy.
Aliueleza Ujumbe wa Viongozi hao wa MCC Overseas kwamba watalii na wageni wanaoingia kwa wingi Zanzibar wakati huu ni wale wanaotoka katika Mataifa ya Ulaya hasa Nchi ya Italy.
Alielezea faraja yake kutokana na Shirika la Ndege la Uturuki hivi karibuni kusaini mkataba wa Ndege zake kuanzisha safari za moja kwa moja kutokea Nchini Uturuki hadi Zanzibar.
“ Tumeshuhudia hivi karibuni utiaji saini Mkataba uliofungwa na Uongozi wa Shirika la Ndege la Uturuki kuanzisha safari za ndege zake moja kwa moja hadi Zanzibar kitendo kinachotuonyesha mabadiliko ya watalaii watakaoingia Zanzibar badala ya wale pekee tuliyowazoea kutoka Italy ”. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Kampuni hiyo ya MCC - Overseas kwa hatua yake ya awali ya kuanza kwa matengenezo ya Ujenzi wa mradi wa Hoteli ya Amber Resort uliyopo Matemwe.
Balozi Seif alifahamisha kuwa mbali ya kuongeza Mapato ya Taifa lakini pia kuanza kwa harakati hizo kutatoa fursa za ajira kwa Vijana wazalendo zinakazowasaidia kupunguza ukali wa maisha.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni