Tangakumekuchablog
Tanga, MICHEZO ya tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) yamemalizika kwa timu ya Bandari ya Tanga kuibuka Mabingwa wa jumla.
Timu ya Bandari ya Tanga imeibuka kwa kunyakua vikombe 7 ikifuatiwa na Bandari Makao Makuu Dar es Salaam kwa kujinyakualia vikombe 7 ambapo Bandari Mtwara na Bandari za Maziwa kila mmoja kujinyakulia kikombe kimoja kimoja.
Akikabidhi vikombe na zawadi mbalimbali kwa washindi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana ,aliwapongeza washiriki hao kwa kuonyesha umahiri katika michezo mbalimbali.
Alisema mbali ya umri wao kwenda juu lakini walikuwa wakionekana kama vijana ambao wanaweza kucheza timu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.
“Nimefarijika kuwaoma wafanyakazi wenzangu umri tofauti mukicheza mpira na kushindwa kutofautisha kijana na mzee, munakimbia uwanjani kama Messi na Ronaldo” alisema Msabimana
Aliwataka wanamichezo hao ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kuwa wamoja na kuwa na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo waliojiwekea.
Mshindi wa bao kutoka Bandari Makao Makuu Dar es Salaam, Mwinyi Sultan, akikabidhiwa kombe na Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana baada ya kuibuka msindi wa mchezo huo wakati wa michezo iliyofanyika Tanga kwa siku 4 viwanja mbalimbali Mkoani humo.
Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, Netboll, kurusha Tufe, kuvuta kamba na riadha wakishangilia ushindi wa jumla mara baada ya kukabidhiwa kombe lao na Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mussa Msabimana. Bandari Tanga imeibuka mshindi wa jumla na kunyakua vikombe 6.
Wachezaji wa timu ya Bandari Makao Makuu Dar es Salaam wakishangilia ushindi mara baada ya kukabidhiwa vikombe vyao kwa michezo mbalimbali, Bandari Makao Makuu walinyakua vikombe 7.
Raha ya Ushindi Bandari Mkao Makuu.Dar es Salaam
Blog ya kijamii tangakumekucha 0655 902929
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni