Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam na Makao Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47.
Wachezaji wa kuvuta kamba timu ya Bandari ya Tanga wakichuana dhidi ya Makao Makuu mchezo umalizika kwa Tanga kuibuka na ushindi wa seti 2-0 mchezo uliochezwa viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly mjini Tanga.
Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam na Makao Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47.
TIMU ya Mpira wa Pete ya Bandari ya Tanga leo wameweza kuibuka na ushindi wa mabao 43-16 dhidi ya Bandari ya Mtwara kwenye michuano ya Bandari inayoendelea mjini Tanga.
Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye viwanja vya Bandari mjini hapa ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko Bandari Tanga ilikuwa ikiongozwa kwa mabao 23 -17 dhidi ya Mtwara.
Halikadhalika Tanga wakiweza kuibuka pia na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini hapa.
Katika mchezo mwengine uliochezwa kwenye uwanja huo timu ya Bandari ya Dar es Salaam iliweza kuibuka na ushindi dhidi ya Makao Makuu kwa mabao 36-13.
Wakati huo huo,Timu ya Bandari ya Dar es Salaam imeweza kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye dimba hilo la Bandari mjini hapa.
Kwenye mchezo mpira wa miguu uliozikutanisha Bandari Mtwara na Maziwa Makuu ambapo timu hizo mpaka dakika 90 zilijikuta zikigawana pointi moja moja baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Ili kuonyesha wana umahiri mkubwa kwenye michezo Bandari Tanga wanaume waliweza kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa kuvuta kamba.
Wakati wanaume wakiibuka na ushindi huo wanawake nao waliweza kuwaunga mkono wenzao kwa kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao makuu kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly.
Mashindano hayo ambayo yalifunguliwa jana na Mkurugenzi wa Bandari nchini (TPA) Deusdedit Kakoko ambaye aliwataka wanamichezo hao kuzingatia nidhamu na maarifa kwenye michezo yao ili kupata ushindi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni