Bondia Anthony Joshua ambaye bado
hajapata changamoto kubwa katika mapambano yake aliyopigana,
ameonyesha kutobweteka kwa kuendelea kujifua zaidi.
Ikiwa zimebakia siku nne kabla ya
kutetea kwa mara ya pili ubingwa wake wa uzito wa juu wa mkanda wa
IBF, bondia huyo Muingereza ameachia picha za mazoezi akinyanyua
vyuma kwa meno.
Joshua ametoa video kwenye mitandao
ya jamii inayomuonyesha akinyanyua kwa kutumia meno vyuma viwili
vizito vyenye umbo la birika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni