Mchezaji Carlos Tevez amekamilisha
uhamisho kuhamia timu ya Shanghai Shenhua na kuwa mwanasoko
anayelipwa mshahara mkubwa kuliko wote duniani wa paundi 615,000 kwa
wiki.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa West
Ham, Manchester United na Manchester City ameingia katika orodha ya
nyota wanaojiunga na ligi tajiri ya China ya Supa Ligi, akitokea Boca
Juniors.
Tevez, 32, atafanyiwa vipimo vya
afya kabla ya kujiunga na wachezaji wenzake wa baada ya kufikia
makubaliano ya maslahi yake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni